Huku
maonyesho ya kilimo ya mwaka huu mjini Eldoret yakiingia siku yake ya tano,
maonyesho hayo yameshuhudia mfuriko wa watu mbalimbali wakiwemo wasimamizi wa
wizara ya kilimo, vyuo vikuu mbalimbali miongoni mwao chuo kikuu cha moi na
wanafunzi kutoka shule za upili na za msingi mbalimbali.

Picha wanafunzi
wakifahamishwa kuhusu saana ya uanahabari.
Maonyesho
hayo yalifunguliwa rasmi juzi jumatano naye gavana wa kaunti hii mheshimiwa
bwana Jackson Mandago ambaye alikisihi chuo kikuu cha moi kushirikiana kwa
ukaribu na serikali ya kaunti hii ili kukuza viwanda na kuinua uchumi wa
kaunti kwa ujumla. Mandago aliongezea
kuwa serikali yake iko tayari kufadhili miradi yote inayolenga kuinua viwanda
na kukitaka chuo kikuu cha moi kizidi kukuza wataalam watakao saidia viwandani.
Huku hayo
yakijiri Mkuu wa makatibu katika sekta ya kilimo bwana Fred Sigor aliyekuwa
mgeni mheshimiwa katika maonyesho hayo hapo jana, alifurahishwa na jinsi
wananchi walivyojitokeza na kuonyesha ujuzi wao katika kilimo.
picha mkuu wa
makatibu wa kilimo bwana Fred Sigor (katikati) akifahamishwa kuhusu shule ya
sayasi ya habari ya chuo kikuu cha moi.
Aidha Sigor alisema
kuwa nivizuri wakulima kuekeza katika mimea inayoweza kukimu mvua chache
kama vile mihogo na viazi tamu kwani misimu ya mvua imekuwa ikishuhudia mvua
chache kitika miaka ya hivi karibuni.
Kosgei
aliongezea kuwa maonyesho ya mwaka huu yamelenga pakubwa kueneza technolojia
katika ukulima na pia kuhusisha vyuo vikuu katika kuelimisha kuhusu ukulima wa
kisasa.