Friday, 6 March 2015

Viongozi wajitokeza katika maonyesho mwaka huu




Huku maonyesho ya kilimo ya mwaka huu mjini Eldoret yakiingia siku yake ya tano, maonyesho hayo yameshuhudia mfuriko wa watu mbalimbali wakiwemo wasimamizi wa wizara ya kilimo, vyuo vikuu mbalimbali miongoni mwao chuo kikuu cha moi na wanafunzi kutoka shule za upili na za msingi mbalimbali.
 
Picha wanafunzi wakifahamishwa kuhusu saana ya uanahabari.
Maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi juzi jumatano naye gavana wa kaunti hii mheshimiwa bwana Jackson Mandago ambaye alikisihi chuo kikuu cha moi kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya kaunti hii ili kukuza viwanda na kuinua uchumi wa kaunti  kwa ujumla. Mandago aliongezea kuwa serikali yake iko tayari kufadhili miradi yote inayolenga kuinua viwanda na kukitaka chuo kikuu cha moi kizidi kukuza wataalam watakao saidia viwandani.
Huku hayo yakijiri Mkuu wa makatibu katika sekta ya kilimo bwana Fred Sigor aliyekuwa mgeni mheshimiwa katika maonyesho hayo hapo jana, alifurahishwa na jinsi wananchi walivyojitokeza na kuonyesha ujuzi wao katika kilimo.
picha mkuu wa makatibu wa kilimo bwana Fred Sigor (katikati) akifahamishwa kuhusu shule ya sayasi ya habari ya chuo kikuu cha moi.
Aidha  Sigor alisema  kuwa nivizuri wakulima kuekeza katika mimea inayoweza kukimu mvua chache kama vile mihogo na viazi tamu kwani misimu ya mvua imekuwa ikishuhudia mvua chache kitika miaka ya hivi karibuni.
Kosgei aliongezea kuwa maonyesho ya mwaka huu yamelenga pakubwa kueneza technolojia katika ukulima na pia kuhusisha vyuo vikuu katika kuelimisha kuhusu ukulima wa kisasa.