Wednesday, 18 February 2015

WASHA TUPATE MWANGA.

“WASHA TUONEE”
Sylvia kadzo
Haya ni maneno ya wanafunzi wakaazi wa nyumba za C almaarufu C houses baada ya kuwasha moto nakuteketeza baadhi ya sehemu za ua wao hapo jana usiku, ilikulamikia ukosefu wa nguvu za umeme kwa majuma kadhaa tangu kuanza kwa muhula huu.
 
Figure 1picha ya moto ulioteketeza sehemu ya ua wa nyumba za C.
Wanafunzi hao waliojawa na ghadhabu walikua wakilalamikia shida ya umeme pamoja na hali duni ya usafi katika mazingira yao, hivyo basi kuchukua hatua ya kuteketeza ua wao ili viongozi wa wanafunzi husika wawasikie kilio chao cha muda mrefu nakujibu matakwa yao. Aidha, walilalamikia ukosefu wa usalama kufuatia visa vya wizi walivyovishuhudia hiv imajuzi katika vyumba vyao ikiwemo hata magodoro kuibwa.
Baadhi yao walitaja kuripoti malalamiko yao kwa wasimamizi husika lakini juhudi zao ziligonga mwamba, hivyo basi kutoa mwito kwa Barile Guyo pamoja na Geofrey Omondi kuwatetea.
Miongoni mwa waliofika katika eneo hilo kushuhudia ni pamoja na mkuu wa maswala ya usalama humu chuoni Bwana  Charles Jamanda,  mwenyekiti wa chama cha wanafunzi MUSO, Geofrey Omondi, msimamizi wa usalama na makaazi ya wanafunzi Barille Guyo pamoja na msimamizi wa maswala ya fedha na mapato ya wanafunzi Seleb John Kenga..
Kufuatia malalamiko ya wanafunzi hao Bwana Guyo alijitetea nakusema kuwa amekuwa akishuhulikia swala hilo na wamekua wakiweka kebo mpya maneo hayo ila kwa ajili ya utumiaji zaidi wa umeme unaozidi nguvu za kebo hizo, zimekua zikiungua kila mara. Aidha Guyo aliongezea kuwa wako katika harakati pamoja na shirika linalosimamia nguvu za umeme nchini KPLC kutoa suluhu kwa tatizo hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ,MUSO bwana Omondi alisema kuwa anafahamu shida ya umeme ni donda sugu humu chuoni na kuwa wameweka mikakati kabambe ilikuhakikisha suluhu inapatikana. Aliongezea kuwa nyaya na kebo zinazohitajika ili kumudu matumizi ya umeme kwenye madahalia yote zinagharimu takriban shilingi milioni 3.5, na kwamba yuko mbioni kushinikiza usimamizi wa chuo kuzinunua bidhaa hizo.
Aidha viongozi hao waliwaomba wanafunzi wote kuwa na subra na pia kuzuia vurugu lolote nakuwaahidi wakaazi wa nyumbaza C kupata umeme wakuweza kuipa mianzi yao mwanga hapo kesho ilhali umeme wakuweza kuwasha majiko yao nakupikia utatamatika ifikapo ijumaa.
Moto huo uliweza kukabiliwa na baadaye kuzimwa na wanafunzi waliojitolea akiwemo msimamizi wa maswala ya fedha na mapato ya wanafunzi, Bwana Seleb John Kenga. Pamoja na maafisa kadhaa wa usalama humu chuoni.

No comments:

Post a Comment