Wednesday, 11 June 2014

MGOGORO WA TSA NA MUSO

Viongozi wa TSA  wamelalamikia vikali kutengwa  kwao na  muungano wanafunzi  wa MUSO  pamoja afisi kuu za utawala za hapa chuoni.
Akiongea na wanahabari aliyekuwa  mwenyekiti wa TSA bwana Fredrick Orem amesema kuwa afisi za utawala zimekuwa zikiwanyima  wanafunzi wa shule teknolojia  haki yao ya kidemokrasia kwani kila mipango ya kuwachagua viongozi wa wanafunzi inaporatibiwa basi wanafunzi wa TSA huwa hawapo shuleni.
Orem aliongezea kuwa chama cha MUSO pia kimekuwa kikiwatenga TSA katika kupanga miradi inayowahusu wanafunzi wote kwa jumla.

Aidha Orem alijiweka wazi na kusema  kuwa yupo tayari kushirikiana na mwenyekiti na viongozi wateuliwa wote ili kuwasilisha lalamiko lao kwa afisi kuu za utawala wa humu chuoni.

2 comments: